Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mara paaap umeshinda MILIONI 40 Tanzania !! imewatokea Mutalemwa na Gibson

Mon, 22 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Watanzania wawili akiwemo Fundi ujenzi wa Mwanza aiwate Gibson Greshen ( ambae kwa sasa yuko Musoma kikazi) na Brighton Mutalemwa wa Songea Mkoani Ruvuma wameibuka Washindi wa Shilingi milioni 40 kila mmoja.

Ni kwenye bahati nasibu kubwa ya Tanzania iitwayo TATU MZUKA ambayo Jumapili ya January 21 2017 ilikua ikitoa zaidi ya milioni 80 kwenye round zote mbili zilizo kwenye utaratibu wa kawaida.

Gibson angeweza kuchukua zote milioni 80 kutoka kwenye round ya kwanza kama Mutalemwa angeshindwa kuotea kadi zote 3 za MZUKA kwenye round ya pili ambako kulimfanya agawane hizo 80 na Gibson.

Ukiachia Gibson na Mutalemwa, kuna Washindi wengine wawili waliojishindia kila mmoja Shilingi MILIONI 27 kutoka kwenye round ya kwanza na ya pili ambao ni Emmanuel Adolph Shayo wa Pugu Ilala Dar es salaam na Andrew wa Sekei Arusha.

Chanzo: millardayo.com