Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapya yaibuka vitambulisho vya wamachinga

Maboresho Vitambulisho Machinga Mapya yaibuka vitambulisho vya wamachinga

Fri, 19 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapya yameibuka baada ya Mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi kuitaka Serikali itoe majibu ya kuwa vitambulisho vya Wamachinga vilivyotolewa kati ya 2016 na 2021, havikuwasaidia.

Shangazi ametoa kauli hiyo leo Mei 19, 2023 bungeni baada ya majibu ya serikali katika swali la msingi alilouliza kuhusu vitambulisho vya wamachinga.

Katika swali hilo la msingi, Shangazi aliuliza ni Wamachinga wangapi wamefuzu kuwa wafanyabiashara rasmi kwa kipindi cha kuanzia 2016 hadi 2021.

“Kwa majibu haya, je Serikali inakiri wazi kuwa vitambulisho vile havikuwasaidia kitu wamachinga wetu hapa nchini,” amehoji Shangazi.

Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesema hadi kufikia Machi 2023 kuna jumla ya machinga 1,987,361 nchini.

“Kwa sasa Serikali inaandaa utaratibu wa kuwatambua wamachinga waliofuzu kuwa wafanyabiashara mara baada ya kurasimisha biashara zao,” amesema Kigahe.

Naibu Waziri huyo amesema Serikali inaendelea kuhamasisha urasimishaji wa biashara nchini kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya faida za urasimishaji biashara kupitia mafunzo mbalimbali ya biashara na ujasiriamali.

Amesema mikakati iliyopo sasa ni uanzishwaji wa vituo jumuishi vya urasimishaji wa biashara na uandaajinwa mwongozo wa taratibu za kurasimisha biashara nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live