Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapinduzi ya bandari yanavyopaisha uchumi

A89ef59e7651c39ec5e074a9045c5317.jpeg Mapinduzi ya bandari yanavyopaisha uchumi

Sat, 16 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bandari ya Tanga inatarajiwa kuanza kupokea meli za magari kuanzia mwezi Mei, mwaka huu. Hatua hiyo inatajwa kwamba itafungua fursa mpya za kiuchumi kwenye bandari hiyo ambayo kwa sasa inafanyiwa maboresho makubwa ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zake.

Hayo yalisemwa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Mrisha Masoud wakati wa ziara ya wadau wa bandari hiyo walipotembelea baada ya kumaliza kikao chao na mamlaka hiyo.

Masoud alisema magari hayo yatatunzwa eneo la Mwambani lenye ukubwa wa hekta 176. Alisema wanatarajia kuhudumia shehena kubwa kutoka tani 750,000 za sasa mpaka kufikia 3,000,000. Akielezea maboresho yalivyofanyika alisema yalihusisha kuongeza kina cha maji kutoka mita tatu mpaka mita 13 kwenye mlango wa bahari, sehemu ya kugeuzia meli na vifaa uligharimu Sh bilioni 172.3. Alisema pia wamefanya maboresho ya gati mbili, zote zikiwa na urefu wa mita 450 zilizogharimu Sh bilioni 256.8.

Alisema kwa ahadi mkandarasi mpaka mwezi Mei mwaka huu watakabidhiwa kipande cha mita 150 na itakapofika Oktoba watakabidhi mita zote 450. Hata hivyo, alisema kwamba hoja ambazo zimewasilishwa na wadau kwenye kikao hicho wamezichukua na wanakwenda kuzifanyia kazi.

Aliwaambia waandishi wa habari kwamba walitumia kikao hicho kuwaeleza wadau maboresho makubwa yaliyofanyika na wao kuahidi kuitumia kwa ajili ya kupitisha shehena zao. Awali akizungumza mara baada ya ziara ya wadau hao, Kaimu Mkurugenzi wa masoko na Uhusiano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Makao Makuu, Nikodemas Mushi alisema mkutano huo ulikuwa na nia ya kukutana na wadau wanaohudumiwa na Bandari ya Tanga ambayo inahudumia mikoa ya Kanda ya Kaskazini ikiwemo nchi jirani ya Rwanda.

Alisema kupitia mkutano huo wanaamini watafungua ukurasa mpya wa kibiashara na lengo lao ni kuondoa nafasi ya maswali, hoja na changamoto mbalimbali ambazo hazijawahi kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live