Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapato yatokanayo na bandari yafikia Bilioni 531.1

Msigwa?fit=1024%2C683&ssl=1 Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa

Mon, 30 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapato ya bandari katika kipindi cha miezi 6 yameongezeka kutoka shilingi Bilioni 525.4 hadi kufikia shilingi Bilioni 531.1, ambapo baadhi ya nchi zimeshindwa kufikia makusanyo hayo kutokana na changamoto ya Korona.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema hayo Dodoma alipokutana na waandishi wa habari na kudai kuwa, Biashara ya bandari inaendelea kukuwa kwa Watanzania na nchi jirani ambazo zinategemea bandari za Tanzania hasa Bandari ya Dar es Salaam.

"Ongezeko kubwa tumelipata katika bandari yetu ya Dar es Salaam ambayo inafanya vizuri kwa kuongeza kiwango cha shehena ya mizigo kutoka tani Milioni 7.270 hadi kufikia tani Milioni 8.136". Amesema Msigwa.

Amesema, Katika miezi 6 iliyopita Februari – Julai, bandari zilizopo ukanda wa Bahari ya Hindi Dar es Salaam, Tanga na Mtwara na Bandari zilizopo katika ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa zimeongeza idadi ya meli kutoka meli 1,388 hadi kufikia meli 2,206. Hali hiyo imeongeza kiwango cha shehena ya mizigo kutoka tani Milioni 7.826 hadi kufikia tani Milioni 8.869.

Hali ya bandari nchini Tanzania inatajwa kuwa nzuri kutokana nakueendelea kutoa huduma ya kusafirisha na kupokea mizigo ndani ya nchi na nje ya nchi licha ya dunia kukabiliwa na janga la Uviko-19.

Ongezeko hilo limetokana na uboresha wa bandari ya Dar es Salaam ulioanza kufanyika mwaka 2016 na kuigharimu serikali gharama ya takribani shilingi Trilioni 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live