Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapato yanayotokana na Utalii yazidi kupaa

8256 Watalii Tz 1 1 TZW

Tue, 22 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 2,131.57 kwa mwaka 2016 hadi kufikia Dola za Marekani 2,250.3 kwa mwaka 2017 ikiwa ni sawa na asilimia 5.6.



Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019.

“Idadi ya watalii walioingia nchini imeongezeka kutoka watalii 1,284,279 kwa mwaka 2016 hadi kufikia watalii 1,327,143 kwa mwaka 2017, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.3. Watalii kutoka Marekani wameongoza katika kuitembelea Tanzania wakifuatiwa na nchi za Uingereza, India, Uholanzi na Uswisi,” amesema Dkt. Kigwangalla.

Ameendelea kusema, mafanikio hayo yanatokana na ujenzi wa miundombinu ya barabara, kuongezeka kwa kasi ya kuboresha na kutangaza vivutio vya utalii, kuimarishwa kwa mifumo ya ukusanyaji madhuhuli na kudhibiti matukio ya ujangili na matumizi yasiyo endelevu ya maliasili na malikale.

Vile amesema, katika juhudi za kutangaza utalii, Wizara imeendelea kutekeleza mikakati mabalimbali ikiwemo kuandaa utambulisho wa Tanzania Kimataifa (Destination Branding). Lengo ikiwa ni kuitambulisha Tanzania kama kituo mahsusi cha utalii Duniani.

Aidha, Wizara hiyo inashirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuanzisha chaneli maalum katika Televisheni ya Taifa (TBC 1) kwa ajili ya kutangaza utalii ambapo kwa sasa Wizara inaendelea na maandalizi ya kuanzisha studio ya kutangaza utalii kwa njia ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Loading...
Chanzo: bongo5.com