Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapato ya madini yaongezeka nchini

Madini Pic Data Mapato ya madini yaongezeka nchini

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“Takwimu zinaonesha kuwa, kuanzia mwezi Machi, 2019 hadi kufikia mwezi Juni, 2022 usimamizi wa masoko ya madini nchini umeendelea kuimarika ambapo kiasi cha kilogramu 51,539.61 za dhahabu; karati 58,747.78 za madini ya almasi; kilogramu 606,253.82 za madini ya bati; kilogramu 284,670.66 na karati 344,370.28 za tanzanite; na kilogramu 10,985.79 na karati 65,033.72 za madini ya vito mbalimbali kiliuzwa kupitia masoko hayo na kuipatia Serikali jumla ya Shilingi bilioni 422.32.

Mheshimiwa Naibu Spika, uchambuzi wa Kamati umegundua kuwa, mchango wa mapato yatokanayo na masoko ya madini umeongezeka kutoka asilimia 2.62 toka kuanzishwa kwake hadi kufikia asilimia 28.36 katika Mwaka wa Fedha 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 25.74. Kamati inaipongeza sana Wizara kwa jitihada hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati inaipongeza Wizara kwa jitihada hizi kwani zitasaidia katika kuhakikisha Taifa na wananchi kwa ujumla wananufaika na rasilimali ya madini.” Mhe. Seif Gulamali Mbunge wa Manonga akisoma taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge Nishati na Madini kwa niaba ya Mwenyekiti Mhe. Dunstan Luka Kitandula

Chanzo: www.tanzaniaweb.live