Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapato ya DART (Mwendokasi) yaongezeka

Dart Pic Data Mapato ya DART (Mwendokasi) yaongezeka

Tue, 30 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imesema mapato ya Mradi wa Mabasi yaendayo kwa haraka jijini Dar es Salaam (DART) yameongezeka kutoka Sh25 bilioni mwaka 2020/2021 hadi kufikia Sh36 bilioni mwaka 2021/2022.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jerry Silaa ameyasema hayo jana Jumatatu Agosti 29, 2022 mara baada ya PIC kuchambua taarifa ya Wakala wa DART.

Amesema mafanikio hayo yametokana na kurejeshwa kwa mfumo wa ukataji wa tiketi kwa njia ya kieletroniki ambao hivi sasa unatumika wa Serikali.

“Kikubwa kamati imeendelea kuwapongeza utakumbuka UDART ilipoanza ilikuwa na tiketi za kieletroniki baadaye ikaingia katika tiketi za mkono lakini sasa wamerudi katika mfumo wa kieletroniki,”amesema.

Aidha, Silaa amesema mkataba kati ya Serikali na mwendeshaji mpya wa DART kutoka Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) utasainiwa Septemba mwaka huu.

Advertisement Silaa amesema hivi sasa mradi huo umekuwa ukiendeshwa kwa mpito na kampuni ya Usafirishaji jijini Dar es Salaam (UDART).

Amesema maelekezo ya kamati kwa wakala wa DART ni kuendelea kusimamia mapato ya kieletroniki, kuboresha utendaji na kukamilisha mchakato wa kumpata mwendeshaji mpya.

“Tumeagiza huyu UDART ambayo ni kampuni ya wazawa na inamilikiwa na Serikali kumtengenezea mshindani, ukimtengenezea mshindani wananchi watanufaika ubora wa services (huduma), unauli na hata huduma wanazozipata zitakuwa zinaenda vizuri zaidi,”amesema.

Amesema kwasasa kampuni hiyo inaendesha vizuri awamu ya kwanza ya mradi huo ambayo ni kuanzia Kimara kwenda Posta wakati awamu ya pili ya Mbagala hadi Kariakoo ikiwa katika ujenzi.

Silaa amesema awamu ya tatu ya kutoka Kariakoo hadi Gongo la Mboto ambayo mkandarasi wa ujenzi wa miundombinu ameshapitikana tangu Machi mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live