Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapato Stendi ya Magufuli sasa Sh Mil 8 kwa siku

Mapato Stendi ,aghufu;li Mapato Stendi ya Magufuli sasa Sh Mil 8 kwa siku

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapato ya jumla ya Stendi ya Magufuli iliyopo jijini Dar es Salaam yemeongezeka kutoka Sh 7,165,100 kwa siku hadi hadi Sh 8,244,100 kwa Siku.

Taarifa ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imesema hiyo ni sawa na ongezeko la Sh 1,079,000 kwa siku.

Taarifa hiyo imesema hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Innocent Bashungwa alipofanya ziara yake kwenye stendi hiyo Mei 30, 2022 na kutoa maelekezo kuhusu uboreshaji wa mapato.

“Maeneo yanaonekana kufanya vizuri ni viingilio vya getini, ushuru wa choo pamoja na adhabu mbalimbali,” imesema taarifa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live