Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maonyesho ya sabasaba yaanza, Veta yaonyesha ubunifu mashine ya kufungashia nyasi

64847 Veta+pic

Sat, 29 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ili kuondoa adha ya upatikanaji wa nyasi kama chakula cha mifugo hasa wakati wa kiangazi na maeneo ya mijini, Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) mkoani Singida kimetengeneza mashine maalumu ‘Hay Baling machine’ kwa ajili ya kufungashia nyasi hizo.

Mashine hiyo ina uwezo wa kufungasha uzito tofauti kulingana na mahitaji ya mteja na haitumii nishati yoyote.

Akizungumzia leo Jumamosi Juni 29, 2019 katika maonyesho ya kimataifa ya biashara sabasaba jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, Mkufunzi wa chuo hicho, Clophas Mkungu amesema uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuona wafugaji katika mkoa wa Singida wanapata tabu ya kupata malisho ya mifugo yao hasa wakati wa kiangazi.

“Muda huo mifugo mingi huwa inadhoofu kwa kukosa chakula cha kutosha lakini wengine majani wanayohifadhi huwa yanaharibika kutokana na kuwekwa katika mfumo usiofaa, hivyo njia hii ni nzuri kwao lakini ukiziweka hivi zinaweza kukaa hata miezi sita.”

“Lakini mashine hii pia inaweza kufungasha Tumbaku au pamba na kupunguza uhitaji wa kuwa na watu wengi ili kuweza kuwafanya kazi hiyo na badala yake mmoja au wawili wanatosha na zinauzwa kati ya Sh250,000 hadi Sh500,000” amesema Mkungu

Akielezea namna inavyofanya kazi, mwanafunzi kutoka chuo hicho, Carlos Kofia amesema ili kutunza nyasi hizo ni lazima pia uwe na kamba ambazo zitaambatanishwa katika nyasi hizo.

Pia Soma

“Kamba hizi za katani ndiyo zitatumika kufunga mzigo wa nyasi, tumbaku au pamba, kuna sehemu ambayo unazichomeka katika upande wa kushoto na kulia na kuzitoa katika tundu la chini na baada ya kuweka mzigo wako utakandamiza vizuri kisha kuchomoa kamba hizo na kulinganisha na ile ya chini unafunga kwa nguvu na mzigo wako unakuwa tayari.”

Amesema mbali na kutunza nyasi hizo kwa ajili ya msimu wa ukame lakini pia watu wanaweza kuitumia kama fursa ya kibiashara kwa sababu wataweza kusafirisha kwenda sehemu yoyote kwa utaratibu maalumu.

“Ukiweka katika utaratibu huu nyasi haziharibiki kwa sababu zinakuwa zimeachiana nafasi na hewa inapita sababu kitu kingine kinachofanya nyasi ziharibike ni joto na unyevunyevu,” amesema Kofia.

Chanzo: mwananchi.co.tz