Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maonyesho ya biashara ya sabasaba kuanza Juni 28

63333 Pic+sabasaba

Wed, 19 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Maonyesho ya 43 ya  kimataifa ya biashara  ya Dar es Salaam.  (DITF) yanatarajia kuanza Juni 28 hadi Julai 13, 2019 kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania  (Tantrade) imezialika kampuni, wananchi, taasisi mbalimbali kutembelea maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es SalaaM (DITF) yanayotarajia kuanza Juni 28 hadi Julai 13 kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, vilivyopo jijini Dar es Salaam.

Tantrade imeeleza kuwa  kauli mbiu ya maonyesho hayo mwaka huu ni ‘Usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda’.

Kabla ya mwaka 2017,  maonyesho hayo yalikuwa yakifanyika kwa siku nane, Julai 2, 2017 Rais wa Tanzania John Magufuli alipokuwa akifungua maonyesho hayo  alimwomba Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania   (Tantrade) Christopher Chiza  afikirie kuongeza siku ili wananchi waweze kushiriki kwa muda mrefu zaidi.

Akijibu ombi la Rais , Chiza alitangaza kuongeza siku tano ambapo maonyesho hayo badala ya kumalizika Julai nane, sasa yatakuwa yakimalizika Julai 13 kila mwaka.

Mwaka jana kampuni zaidi ya 2000 za ndani na nje  zilishiriki maonyesho hayo, pia nchi 30 na taasisi za Serikali zaidi ya 100 zilishiriki.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz