Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maonesho ya Sabasaba kuonesha fursa za madini nchini

Maonesho Ya Sabasaba Kuonesha Fursa Za Madini Nchini.jpeg Maonesho ya Sabasaba kuonesha fursa za madini nchini

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini itatumia Maonesho mbalimbali nchini kutangaza na kuonyesha fursa mbalimbali zilizopo kwenye Sekta ya Madini ikiwemo uchimbaji ili Watanzania na Wadau wanufaike na rasilimali hiyo.

Hayo yamebainishwa leo Juni 30, 2023 na Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga wakati akitembelea mabanda ya Wizara ya Madini, Taasisi pamoja na wadau wake katika Maonesho ya 47 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

"Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameona kuna umuhimu wa kufanya maonesho haya kwa nguvu kubwa sana ili watu waweze kujua hizi fursa zinazopatikana katika Sekta ya Madini," amesema Dkt. Mwanga.

Ameongeza kuwa, Sekta ya Madini inamchango mkubwa kwenye upatikanaji wa fedha za kigeni ambapo zaidi ya asilimia 50 ya fedha zote za kigeni zinazopatikana nchini zinachangiwa na mauzo ya Madini nje ya nchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwema wa Kampuni ya Tanzakwanza Francis Daudi inayojihusisha na maandalizi ya maonesho ya 47 ya Sabasaba ameipongeza Wizara ya Madini na Taasisi zake pamoja na wadau kwa kupewa kipaumbele katika maonesho hayo na wizara.

Naye, Meneja wa Mawasiliano na Uhamasishaji kutoka Chemba ya Migodi Muki Msami amesisitiza ushiriki wa Kampuni kubwa na za kati za uchimbaji kushiriki katika makongamano mbalimbali ya madini ili kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika migodi yao.

Dkt. Mwanga ametembelea mabanda ya Taasisi za Wizara ya Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) pamoja na banda la Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM), Peak Rare Earths, Tanzania Chamber of Mines, Jitegemee Holdings Ltd, Yaya Resources, Mkonya Investment Ltd, Mining Services Ltd ili kujionea shughuli zinazofanywa na kampuni hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live