Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manyanya ataka SIDO kuendeleza ushirikiano na waleta vifungashio

7669754cfe50488af18d62aa00a15ed0 Manyanya ataka SIDO kuendeleza ushirikiano na waleta vifungashio

Mon, 10 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya amelitaka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo( SIDO) kuendelea kushirikiana na wafanyabiashara wanaoagiza vifungashio ili kuondoa changamoto za upatikanaji wake.

Alisema hayo juzi wakati alipotembelea banda la SIDO kwenye viwanja vya Maonesho ya Wakulima, Wafu gaji na Wavuvi maarufu Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma. Alisema upatikanaji wa vifungashio ilikuwa ni tatizo kubwa la wajasiriamali lakini sasa SIDO wamekuwa wakishirikiana na wauzaji wanaoagiza vifungashio, hivyo kupunguza tatizo la upatikanaji wake.

“Siku za nyuma ilikuwa watu wengi wakiuza bidhaa kama asali kwa kutumia chupa zilizotumika za konyagi, lakini sasa ukienda SIDO utaunganishwa na wauzaji wa vifungashio,”alisema.

Mmoja wa wauzaji wa vifungashio, Donald Betwala alisema amekuwa akiagiza vifungashio kwa ajili ya bidhaa za aina mbalimbali. “Ninavyo vifungashio vya kutosha na ninapatikana barabara ya nane na pia kwenye soko la Rehema Nchimbi Jijini Dodoma,” alisema.

Pia Manyanya aliwataka wakulima na wasindi kaji wa vyakula kutumia lugha ya kiswahili sanifu katika kutambulisha bidhaa zao walizofungasha ili kumsaidia Mtanzania kujua bidhaa anayotumia.

Akizungumza katika banda la Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) alisema “Tunatakiwa tuwe na utaratibu wa kutambulisha bidhaa zetu kwa Lugha yetu ya Kiswahili, lugha ambayo inaeleweka kwa kila mtu, tuache tabia ya kutamburisha bidhaa zetu kwa lugha za kigeni kiingereza”.

Aliwataka wakulima wote kutambua kwamba maonesho ya mwaka 2021 bidhaa zote zilizofungashwa na kuandikwa kwa lugha ya kiingereza hazitaingia kwenye maonesho hayo.

Hata hivyo alisema serikali imekuwa ikisisitiza wakulima na wachakataji wa vyakula kutumia lugha raisi kwenye bidhaa zao, lakini jambo hilo limeshindwa kutekelezeka.

Chanzo: habarileo.co.tz