Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamlaka ya kusimamia uvuvi bahari kuu yaingiza mapato Sh4.1 bilioni

Uvuvi 23 Mamlaka ya kusimamia uvuvi bahari kuu yaingiza mapato Sh4.1 bilioni

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tangu mamlaka hiyo imeanzishwa mwaka 2010 imeweza kutoa leseni 539 kwa Katika kipindi cha Julai 2022 hadi Februari 2023 Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) imeweza kukusanya Sh4.1 bilioni kutokana na uvuvi wa bahari kuu.

Hayo yameelezwa jana Jumatano Februari 8,2023 Hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Emmanuel Sweke wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo.

Mkurugenzi huyo amesema mwaka 2015-2016 Mamlaka hiyo iliweka rekodi ya kukusanya Sh6.4 bilioni kutokana na kutoa leseni 96 za uvuvi wa bahari kuu.

Amesema tangu Mamlaka hiyo imeanzishwa mwaka 2010 imeweza kutoa leseni 539 kwa kampuni mbalimbali za uvuvi.

“Jamani tukumbuke kwamba hii ni taasisi ya usimamizi sio ya kukusanya mapato lakini tunakusanya mapato kutokana na kazi ambazo tunazifanya mtu akichukua lesini ni lzima atoe fedha,”amesema Mkurugenzi huyo.

Hata hivyo, amesema mwaka 2016 serikali iliamua kufanya maboresho ya sheria lengo likiwa ni kuongeza mapato kwa kuweka mrabaha wa asilimia 0.4 kwa kilo moja ya samaki.

“Sasa baada ya kuweka hiyo kanuni meli nyingi zilikimbia zikabaki chache baadae zikapoteza kabisa,”amesema Mkurugenzi huyo.

Amesema kanuni na sheria zilipobadilishwa mwaka jana serikali ilianza kupata mapato tena kwa kuingiza Sh1.1 bilioni.

“Kuanzia Julai mpaka wiki moja iliyopita tumekusanya Sh4.1 bilioni tumevunja rekodi baada ya miaka takribani saba na tunaendelea.

“Tunafanya kazi kwa bidii mwezi June mwaka huu tutakuwa tumefika Sh6.3 bilioni tunajaribu kuzungumza na wamiliki wa nje wazidi kurudi,” amesema.

Amesema mafanikio ambayo wameyapata ni pamoja na kuwa na mfumo wa kisasa wa kuweza kufuatilia meli popote ilipo na shughuli inayofanya.

“Meli yoyote ambayo tunaipatia leseni lazima iunganishwe katika huo mfumo. Pia kwa sababu ya mazingira yalivyo kuna uvuvi na masuala haramu yanayohusiana na uvuvi,”amesema mkurugenzi huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live