Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo yameiva ununuzi meli za uvuvi

Meli  Uvuviii.png Mambo yameiva ununuzi meli za uvuvi

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Dk. Jim Yonazi amewataka wataalamu waelekezi kutoka Kamapuni za DMG na TANSHEQ walioshinda zabuni ya Mkataba wa Upembuzi Yakinifu wa Ununuzi wa Meli za uvuvi wa Bahari Kuu na Ujenzi wa Viwanda vya Kuchakata Samaki,kukamilisha upembuzi kwa wakati ili Serikali ianze ujenzi wa meli katika Bahari Kuu na Viwanda vya kuchakata samaki.

Dk . Yonazi ametoa kauli hiyo Februari 27,2024 Jijini Dodoma baada ya zoezi la utiaji saini wa Mikataba ya kufanya upembuzi yakinifu wa kijenga Meli za Uvuvi wa Bahari Kuu na viwanda vya kuchakata samaka vitakavyojengwa Kilwa na Fungurefu.

Amesema kuwa Mkataba huo utatekelezwa kwa muda wa siku zisizozidi 45 kwa gharama ya Shilingi milioni 348.

Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi ni ya kimkakati katika kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi, hivyo, katika zoezi hilo la upembuzi yakinifu ni vyema likasimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha linafanyika kwa ufanisi unaotakiwa ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zote zitakazojitokeza.

Amesema kukamilika kwa upembumbuzi yakinifu kwa wakati kutawezesha Serikali kuanza taratibu za ujenzi wa meli za uvuvi katika bahari kuu pamoja na viwanda vya kuchakata samaki vya Kilwa Na Fungurefu.

Kwa upande wake Mratibu wa Programu ya AFDP Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Salimu Mwinjaka amesema kuwa matarajio ya Programu hiyo ni kuwanufaisha watu takribani 1,300,000 ikiwemo kaya za wakulima wadogo 200,000 amabao watakuwa wanapata mbegu bora za mahindi , alizeti na maharage.

Amesema Serikali inakusudia kununua Meli 8 kwa ajili ya uvuvi wa Bahari Kuu ikijumuisha Meli 4 kwa ajili ya TAFICO na Meli 4 kwa ajili ya ZAFICO ambapo Zaidi ya Tsh Bilioni 30 kutumika kununua Meli hizo katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza kutakuwa na Meli 3 na Meli 5 zitanunuliwa katika awamu ya pili na meli hizo zinakusudiwa kuendeshwa kwa njia ya PPP.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live