Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo yaiva biashara hewa ya ukaa

Hewa Ya Ukaaa Ukaa Mambo yaiva biashara hewa ya ukaa

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WIZARA ya Maliasili na Utalii inatarajia kupata dola Bilioni 20 baada ya mazungumzo kuanza kufanyika kati yake na kampuni 22 kwa ajili ya biashara ya hewa ukaa.

Akizungumza katika Mkutano wa fursa zilizopo katika mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo biashara ya hewa ukaa leo jijini Dar es Salaam,Waziri wa Maliasili na Utalii, Angela Kairuki amesema serikali ina misitu ambayo inasimamiwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), kuna mamlaka ya hifadhi ya Misitu na Mamlaka ya wanyamapori (TAWA).

Amesema kupitia taasisi hizo wnaweza kupata fedha zinazoweza kusaidia katika ulinzi, uhifadhi na shughuli za maliasili na utalii.

"Ni fursa kwetu na sasa tupo katika hatua ya mashauriano na kampuni hizo na makubaliano yapo hatua mbalimbali kama yakifanikiwa tunaweza kupa dola bilioni 20 kama wizara na taasisi zake,"amesisitiza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live