Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo ni buli buli mradi wa SGR

SGR 1 Mambo ni buli buli mradi wa SGR

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania(TRC), imemaliza ziara ya kukagua mradi Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha tano kutoka Isaka – Mwanza na kuridhishwa namna kasi ya ujenzi unavyoendelea.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo leo, Meneja mradi msaidizi kituo cha Mwanza -Isaka Moga Kulwa amesema kuwa mradi huo wa ujenzi umefikia asilimia 39.

Amesema katika kipande cha tano cha Mwanza-Isaka kutakuwa na jengo abiria, ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 961 kwa wakati mmoja.

"Mpaka hivi sasa mradi wetu tunategemea ukamilike mwaka 2024 mwezi wa Mei na mradi huu utawasaidia sana wafanyabiashara kwa sababu usafiri huu utakuwa unatumia saa 8 kutoka Mwanza -Dar es Salaam na usafiri wetu utakuwa wa bei ya chini, ‘’ amesema Kulwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRC, Ally Karavana amesema mradi unaendelea vizuri Watanzania watarajie mradi utakamilika kwa wakati.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa TRC, Amina Lumuli amesema lengo la ziara hiyo ni kuipa uelewa bodi mpya ya wakurugenzi kuhusu mradi wa SGR na walianzia kipande cha kwanza cha mradi huo kilichopo Dar es Salaam na kumaliza kipande cha tano Mwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live