Hawa Chimbalanga maarufu Mama Shani ni Mwanamke ambaye amejipatia umaarufu Mkubwa ndani na nje ya Wilaya ya Tunduru kutokana na kazi yake ya upishi na uuzaji wa chakula.
Kutokana na ustadi wake katika mapishi Chimbalanga alipewa jina lingine ambalo ni Mama Ntilie wa kishua amevuna wateja wengi wakiwemo Viongozi wa Serrikali ilayani humo, wafanyabiashara na wananchi. Mwenyewe anasema siri ya mafanikio ni usafi wa kati kazi zake huduma bora, ukarimu na ma upekee wa chakula wa chakula chake.
“Siri ya kuvutia wateja wengi zaidi ni usafi, na huduma bora, upendo, ukarimu na wengi wanapenda vyakula vya asili ambayo Huwa napika na kuviuza katika mgahawa wangu,” anasema.
Kwenye mgahawa wa Mama Ntilie wa kishua anauza supu ya kuku wa kienyeji, wali, ndizi, kande, ugali wa muhogo, wa dona kwa mboga za mlenda na kisamvu. Mama Shani (55) ni mtoto wa kwanza kwa Mama na Baba Chimbalanga amezaliwa katika Kijiji Cha Mbesa Wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma amefanya shuguli hizo kwa muda wa miaka 20 sasa. “Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 20, nilianza kwa kufanya kazi kwa mama deli ambaye alikuwa anamiliki mgahawa ndani ya eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na baadae katika mgahawa wa Mama mwakajinga katika baa ya Camp David“ Mama Shani alianza biashara hiyo baada ya kupata uzoefu Camp David na aliona kuwa shughuli hiyo ndiyo mkombozi wa maisha yake kwani kimasomo aliishia darasa la saba (mwaka 1982). Anasema baada ya kufanya kazi muda mrefu kwa watu aliamua kuanzisha mama Shani mgahawa akiwa na mtaji wa Sh30, 000, lakini imekuwa ikikuwa kila siku na sasa anakubalika, watu wengi wanapa biashara za ukubwa tofauti. “Biashara ya Mama ntilie inalipa ukiifanya kwa nidhamu, imebadili maisha yangu sasa hivi najulikana kwa watu wenye nafasi mbilimbali katika jamii wakiwemo viongozi wa siasa, dini, na hata wafanyabiashara wakubwa ambao wamekuwa wakisaidia kukua zaidi” Anasema zaidi kuwa, biashara hiyo imemsaidia kukidhi mahitaji yake na ya familia kwani kupitia mama ntilie anasomesha watato wake wanne katika ngazi tofauti. Mama Shani ambaye ametoa ajira za kudumia 16 anasema biashara hiyo imemsaidia pia kujenga nyumba ya kuishi, kununua kiwanja na shamba lenye ukubwa wa ekari nne. “Nilianza na mfanyakazi mmoja baadae nikawa naongeza idadi kadri biashara inavyokuwa, hivi ninaposema nina wafanyakazi wa kudumu 16 lakini ukiwema na wale wanaolipwa kwa kutwa jumla ni 40, kati yao wanaume ni 10 na Wanawake 30” Ukiachana na wafanyakazi wa kudumu na wale wa kutwa kunja wakati mama ntilie huyo hutoa kazi hadi kwa watu 100 hususan anapopata tenda za kulisha umati mkubwa wa watu. Hata hivyo pamoja na hatua aliyoipiga bado hajaridhika na mafanikio yake kwani ndoto yake kubwa ni kuwa na hoteli itakayotoa huduma ya vyakula vya asili si tu ndani ya Tunduru. Anafafanua Zaidi kuwa kwa sasa fedha nyingi anayopata huishia kuwalipa wafanyakazi na nyingine huhudumia watoto wake hasa anaye soma huchukua zaidi ya aslinia 60 ya fedha zake, ila hajakata tamaa. Changamoto Mama ntilie wa kishua anasema ni kutotulia kwa wafanyakazi kwani kuna wati inabidi atafute wafanyakazi wapya ndani ya muda mfupi lakini pia ushindani katika biashara hiyo unaongezeka kila siku. “Kuna wakati ikitokea mmekwaruzana na kumsema kesho yake anakwambia anaacha kazi, hapo inabidi kutafuta mwingine kushika nafasi hiyo ili huduma ziendelee. Vilevile kuna changamoto ya kuongezeka kwa ushindani wa kibiashara kutokana na wengi kufungua migahawa jirani na eneo langu lakini napambana kuonyesha tofauti” Anasema, anategemea kufanya vizuri katika biashara yake na hata kufikia kumiriki mali zaidi ikiwa ni pamoja na kumiliki gari yake ambayo ataitumia kwa ajili ya kupeleka chakula kwa wateja wake. Mama Shani anasema kwa sasa anahitaji uwezeshaji wa kifedha zaidi ili kupanua eneo lake la biashara lakini pia vifaa kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma. “Nawashauri wanawake wenzangu wajitokeze kufanya biashara ili kujiondoa kwenye utegemezi ambao hupelekea manyanyaso kutoka kwa watu wanao wategemea,” anasema. Kongamano la Wajasirimali Ili kuwezesha biashara change, za chini, ndogo na za kati kukua haraka, kampuni ya mwananchi Commmunications Limited (MCL) imeandaa kongamano la wadau litakalofanyika Aprili 27 katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam. Mada zitakazojadiliwa katika kongamano hilo ni nafasi ya ubunifu na teknolojia katika kukuza mfumo wa biashara na kuongeza faida na Miradi inayotolewa ufadhili, (Mahitaji na wigo wake). Vivile kutakuwa na ihusuyo kujenga ustahmilivu, (mikakati ya kukabiliana na mtikisiko wa soko kiuchumi) na Mipango ya biashara na programu za kujiendeleza, mbinu bora na rasilimali zinazopatikana kwa biashara za chini, ndogo na za kati (MSEMs) Kadhalika mada nyingine zitahusu Kufungua uwezo wa masoko ya bidhaa nje (Fursa kwa MSMEs kupanua wigo wao) na Kuwawezesha wanawake na vijana wajasiriamali (Kufungua uwezo wa MSMEs katika sekta hiyo nchini).