Menu ›
Biashara
Fri, 7 Oct 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Zaidi ya Malori 600 ya kusafirisha bidhaa kutoka Tanzania kwenda Kenya yamekwama mpakani Namanga kwa zaidi ya wiki moja.
Msururu wa malori umesababisha foleni kubwa na huku madereva wakilalamika kuwa wamekamilisha taratibu zote za kuingia nchini humo lakini magari yao hayajavukishwa kuingia hali inayowasababishia mateso na hasara kubwa.
"Toka jumatatu gari liko ndani lakini bado hawajafanya utaratibu wa kuivusha na kwenye foleni nimemaliza siku tatu upande wa Kenya lakini hadi leo bado sijajua kama gari itavukishwa ama lah,” Martine Mfinanga, dereva wa Lori.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live