Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malori ya bidhaa yakwama kuingia Uganda

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Magari ya mizigo zaidi 50 yaliyosheheni bidhaa kutoka Tanzania, yakwama kuingia Uganda.

Magari hayo yamekwama mpakani Mtukula kwa kile kinachoelezwa kuwa, madereva na wamiliki wa mizigo wameshindwa kumudu kulipia ushuru mpya uliotangazwa na Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA) kwa bidhaa kutoka Tanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, Dennis Mwila amesema leo Jumatatu Juni 11, 2018 kuwa majadiliano kati ya mamlaka za Serikali kutoka Tanzania na Uganda yanaendelea kulipatia ufumbuzi suala hilo.

Emmanuel Tarimo, mmoja wa madereva waliokwama mpakani tangu Juni 8, 2018 amesema wenye shehena ya vitunguu bidhaa zao zimeanza kuharibika kutokana na kufungwa ndani ya magari kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara eneo la Mtukula, Murshid Bazari amesema kukwama kwa wafanyabiashara kuna madhara kwa uchumi wa mataifa haya mawili, akiwaomba viongozi kutafuta ufumbuzi wa haraka.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Deodatus Kinawilo amesema Serikali itatoa ufafanuzi kesho Jumanne Juni 12, 2018 baada ya majadiliano yanayoendelea kukamilika.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz