Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malori 600 yanayotoka Tanzania yadaiwa kukwama Kenya

DSCN5839 Malori Malori 600 yanayotoka Tanzania yadaiwa kukwama Kenya

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zaidi ya Malori 600 ya kusafirisha bidhaa kutoka Tanzania kwenda Kenya yamekwama mpakani Namanga kwa zaidi ya wiki moja.

Msururu wa malori umesababisha foleni kubwa na huku madereva wakilalamika kuwa wamekamilisha taratibu zote za kuingia nchini humo lakini magari yao hayajavukishwa kuingia hali inayowasababishia mateso na hasara kubwa.

"Toka jumatatu gari liko ndani lakini bado hawajafanya utaratibu wa kuivusha na kwenye foleni nimemaliza siku tatu upande wa Kenya lakini hadi leo bado sijajua kama gari itavukishwa ama lah,” Martine Mfinanga, dereva wa Lori.

Dereva mwingine wa lori Hussein Kassim amesema: “Kwanza tumeletwa kwa parking, parking ambayo ni ya vumbi, hamna choo hamna vyakula, halafu tunatakikana tulipe parking shilingi elfu tano ya Tanzania.”

“Exports za Tanzania zimekuwa nyingi lakini ukiangalia utendaji umesalia palepale, tuongeze muda wa kazi tuongeze utendaji tuongeze utumishi,” Transport Manager Abdi Salat amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz