Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malighafi za nyuklia kuzalishwa Pangani

MAVUNDEEEEEE Malighafi za nyuklia kuzalishwa Pangani

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuwezesha upatikanaji wa leseni kubwa ya uchimbaji madini (Special Mining License - SML) kwa Kampuni ya Nyati Mineral Sand inayomilikiwa na kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Strandline ambayo itapelekea kuanza kwa mradi mkubwa wa uchimbaji madini Tembo katika Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga unaotarajia kutoa ajira zaidi ya 1,800.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema hayo leo alipofanya ziara ya kutembelea sehemu ya eneo la mradi huo iliyopo katika Kijiji cha Stahabu, Kata ya Mikinguni Wilayani Pangani-Tanga

“Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Wizara ya Madini kuhakikisha tunawezesha uanzishwaji wa miradi hii mikubwa na ya kimkakati ambayo itapelekea sio tu ustawi wa uchumi wa Nchi yetu, bali kuwa kichocheo cha maendeleo na ustawi wa Wilaya ya Pangani na Wananchi wanaozunguka mradi huu.

Mradi huu unatarajiwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 125 ikiwa ni gharama za awali kabla ya uzalishaji kuanza zikihusisha mchakato wa awali na malipo ya fidia “Mradi huo unakadiriwa kuishi kwa miaka 20 hadi 25 utatekelezwa katika Vijiji 8 vilivyopo katika Kata za Mikinguni, Mwera, Tungamaa na Bweni Wilaya ya Pangani,Mkoani Tanga”

Akiongea kwa niaba ya Mwekezaji, Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyati Mineral Sand Ltd ambaye anawakilisha Hisa za Serikali, Heri Gombera alieleza kwamba mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka 2026 na unatarajiwa kuzalisha tani milioni 8 kwa mwaka ya madini mbalimbali yakiwemo titanium, ilmenite, rutile, zircon na monazite ambayo pamoja na matumizi mengine hutumika pia kuzalisha malighafi za injini za ndege, nyuklia, vifaa vya Hospitali na viwanda vya marumaru na rangi.

Kwa upande wake DC wa Pangani Zainab Abdallah amewaomba Wawekezaji wa viwanda vya tiles, rangi na dawa za meno kwenda kuwekeza Pangani na kuweka viwanda maana kutakuwa na malighafi ya uhakika kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live