Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali ghafi za kioo kupatikana nchini

Dkt Kijaji Awataka Wafanyabiashara Dodoma Kuchangamkia Fursa Mali ghafi za kioo kupatikana nchini

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema uamuzi wa Serikali wa kulipa fidia wananchi wanaozunguka mradi wa madini ya vioo wa Engaruka uliopo wilayani Monduli mkoani Arusha....

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kuunganisha malori na matipa cha Satarn kilichopo Kigamboni mkoani Dar es Salaam, Dkt. Kijaji amesema malighafi zinazopatikana katika mradi huo zitatosheleza kwa zaidi ya asilimia 99 viwanda vya vioo hapa nchini.

Dkt. Kijaji amesema mradi huo ni muhimu kwa uchumi wa viwanda vya vioo na kwamba hakutakuwa na haja ya kuagiza malighafi kutoka nje ya nchi.

Amesema hatua hiyo ya Serikali ni ushindi mkubwa kwa wawekezaji na wazalishaji wa bidhaa za vioo hasa viwanda vilivyopo hapa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live