Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malawi yaruhusu safari mabasi ya Tanzania

A1ec854831543234aaa9df95d05aa101.jpeg Malawi yaruhusu safari mabasi ya Tanzania

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Malawi imetoa ruhusa kwa mabasi kutoka Tanzania kwenda nchini humo kwa kampuni ya Falcon kuanza safari zake tena. Kutokana na uamuzi huo, Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole amewataka wafanyabiashara nchini kutumia fursa hiyo kwenda Lolongwe na kutumia fursa za kiuchumi zinazopatikana nchini humo.

“Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi unapenda kuujulisha umma wa Watanzania kuwa serikali ya Malawi…imeridhia kuanza tena huduma za usafiri wa mabasi kutoka Tanzania kuja Malawi kwa kampuni ya mabasi ya Falcon Executive,” ilisema taarifa ya ubalozi. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, serikali ya Malawi imetoa ruhusa hiyo kupitia Wizara ya Usafirishaji na Ujenzi na Idara yake ya Huduma za Usafiri na Usalama Barabarani kwa uhusiano mzuri na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra).

Ilieleza kuwa mabasi hayo yataruhusiwa kufanya safari zake moja kwa moja mpaka Lilongwe bila kushusha wala kupakia katikati ya njia ndani ya mipaka ya Malawi. Pia kampuni hiyo ya mabasi imetakiwa kuzingatia sheria zote za nchi ya Malawi zinazopaswa kutekelezwa wakati wote wa ruhusa hiyo ikiwa ni pamoja na kufuata ratiba ya utoaji huduma itakayotolewa.

Idara hiyo imewataka pia wafanyakazi na wahudumu wa kampuni hiyo kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na mamlaka za Malawi ili kurahisisha utekelezaji wa huduma hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live