Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malawi yapiga marufuku mahindi ya Tanzania, Kenya

Mbegu Za Mahindi (600 X 349) Malawi yapiga marufuku mahindi ya Tanzania, Kenya

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya na Tanzania kwa muda mrefu wamekuwa vyanzo vikuu vya mahindi kwa Malawi wakati wa vipindi vya uhaba wa chakula lakini sasa Wizara ya Kilimo ya Malawi imetangaza marufuku ya uagizaji bidhaa kutoka nje ya Taifa hilo

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Kilimo ya Malawi imeeleza kuwa uwepo wa ugonjwa wa Mahindi unaosababishwa na Lethal Necrosis ambao hauna tiba ni miongoni mwa sababu inayochochea uwepo wa zuio hilo

Shirika la Habari la Kimataifa la Uingereza (BBC) limechapisha taarifa hiyo kwenye mandao wake na kueleeza kuwa Malawi imepiga marufuku uingizaji wa mahindi kutoka Kenya na Tanzania kutokana na wasiwasi wa kuenea kwa ugonjwa wa Mahindi Lethal Necrosis ambao unaweza kuharibu chakula kikuu kinachotegemewa Malawi wakati huu ambao idadi ya watu milioni Nne (4) katika nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Afrika wanakabiliwa na uhaba wa chakula

Kenya na Tanzania kwa muda mrefu wamekuwa vyanzo vikuu vya mahindi kwa Malawi wakati wa vipindi vya uhaba wa chakula hata hivy Wizara ya Kilimo ya Malawi imetangaza marufuku wiki hii ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje katika taarifa inayosema ugonjwa wa Mahindi unaosababishwa na Lethal Necrosis hauna tiba na unaweza kusababisha hasara ya mavuno kwa asilimia 100

Taarifa hiyo inaendelea kufafanua kuwa Mahindi hayo yanaweza tu kuingizwa nchini humo mara tu yanaposindikwa, ama kama unga au mbegu

Akizungumzia katazo hilo Henry Kamkwamba ambaye ni mtaalamu wa kilimo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Sera ya Chakula amesema hatua hiyo itaisaidia Malawi kujikinga na ugonjwa huo

“Kama mnavyofahamu baadhi ya mbegu tayari zimeharibika kutokana na ukame wa muda mrefu na watu wanapanda kwa mara ya pili, tukiagiza baadhi ya mahindi haya, kuna uwezekano kwamba baadhi ya mahindi ambayo yataingizwa nchini, yanaweza kutumika kama mbegu ingawa hayajapendekezwa kama mbegu" -Kamkwamba

Serikali ya Malawi imesema marufuku hiyo itakuwa ya muda mfupi huku ikichunguza hatua zaidi za kujikinga ili kukabiliana na ugonjwa huo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live