Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makontena ya Makonda kaa la moto bandarini

14996 Makonda+pic TanzaniaWeb

Sat, 1 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mnada wa makontena 20 yaliyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda umefanyika bila mafanikio, baada ya wateja kushindwa kufika bei.

Hii ni mara ya pili kwa makontena hayo kukosa wateja tangu yalipoanza kuuzwa Agosti 25.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ghala la Dar es Salaam Inland Container Depot (DIC) leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono (Auction Mart), Scholastica Kevela alisema wataendelea na mnada hadi makontena hayo yauzike.

"Mnada umekuwa 'very successful' tumeuza mali za aina tofauti tofauti yakiwamo magari na bidhaa nyinginezo. Mnaniuliza makontena mangapi, mimi kwa upande wangu nimeuza kama nilivyopewa maelekezo," alisema na kuongeza:

"Makontena yalikuwa 20 bei imefika hapo ilipofika na tunaendelea na marketing. Kama ilivyosema serikali kwamba huu sio mwisho wa Mnada, kwa hiyo tutaendelea mpaka makontena yote yapate wateja."

Hata hivyo, Kevela alikataa kutaja bei ya mwisho akisema hiyo ni kazi ya Kamishna mkuu wa Mamlaka ya mapato (TRA).

Mbali na makontena hayo, Kevela alisema wameuza bidhaa mbalimbali katika mnada huo na wataendelea nao wiki ijayo.

Soma Zaidi:

Mali makontena ya Makonda zaanza kupigwa mnada

Chanzo: mwananchi.co.tz