Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makontena 1,600 ya makinikia yauzwa nchini

Makinikiapic Makontena 1,600 ya makinikia yauzwa nchini

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini nchini, Dotto Biteko amesema katika kipindi cha Februari 2020 hadi Machi 2021 makontena 1,600 ya makinikia yameuzwa.

Aidha, Biteko amesema katika mwaka wa fedha uliomalizika Juni 2021, mapato yaliyopatikana ya Sh584.8 asilimia 2.5 yalitokana na makinikia.

Biteko ameyasema hayo leo Ijumaa Novemba 5, 2021 wakati akizungumzia mafanikio ya sekta ya madini katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Biteko ameitaja migodi iliyokuwa inazalisha makinikia nchini ni Bulyanhulu na Buzwagi.

Biteko amesema 24 Januari, 2020 walisaini makubaliano ya kuunda kampuni ya Ubia kati ya Serikali na Kampuni ya Dhahabu Barrick ya Twiga.

“Mwezi mmoja baadaye Barrick walileta maombi kuwa wamepata mteja. Katika kipindi hicho hadi kufika Machi 2021 makontena 1,600 yalikuwa yameshauzwa,”amesema.

Amesema pia baada ya kuunda kwa kampuni hiyo walikubaliana kubadilisha mfumo na utaratibu badala ya kuuzwa kama makinikia yauzwe kama madini.

Amesema hivi sasa wanachukua sampuli katika makinikia na kupeleka katika maabara tatu na timu tatu zisizojuana ambazo zinahusika katika kupima makinikia.

Amesema Mgodi wa Bulyanhulu hivi sasa umehama katika uzalishaji wa makinikia na sasa unazalisha vitofali vya dhahabu (block gold) kwasababu ya gharama na masuala mengine.

Amesema katika makinikia hivi sasa wanatoza kila aina ya madini ambapo kabla ya hapo walikuwa wakitoza kwenye dhahabu, Silver na Copper tu.

Amesema wanajua aina na kiasi cha madini yaliyopo katika makinikia na hivyo kutoza inavyotakiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live