Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makinikia ‘yawaliza’ wafanyakazi Acacia

15893 Makinikia+pic TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, imepunguza wafanyakazi kwa kile ilichokiita mabadiliko ya utawala.

Pia, imetaja sababu nyingine za kupunguza wafanyakazi kuwa ni katika mpango wa kupunguza gharama wakati huu ambao Serikali imezuia usafirishaji mchanga wa madini maarufu makinikia.

Hii ni mara ya pili kwa Acacia kupunguza wafanyakazi tangu Serikali ilipozuia usafirishaji wa makinikia.

Serikali ilizuia Acacia kusafirisha makinikia Machi mwaka jana baada ya agizo la Rais John Magufuli kutaka kuhakikisha Serikali inapata mapato ya kutosha katika shughuli za uchimbaji wa madini. Zuio hilo ambalo mpaka sasa halijaondolewa, limesababisha mapato ya kampuni hiyo mwaka 2017 kupungua kwa asilimia 29 ukilinganisha na 2016.

Akizungumza na gazeti hili jana mkurugenzi wa Acacia, Assa Mwaipopo alisema tangazo la punguzo la wafanyakazi ni la kweli.

“Tangazo ni la kweli, ninashangaa tu umepataje habari hizo wakati liliwekwa kwa ajili ya watu wa ndani tu,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu idadi ya wafanyakazi watakaopunguzwa, Mwaipopo hakutaka kufafanua.

Hata hivyo, tangazo hilo limefafanua kuwa upunguzaji huo utafuata taratibu za sheria za kazi na majadiliano baina ya wafanyakazi na uongozi.

Chanzo: mwananchi.co.tz