Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makandarasi waiomba Serikali ya Tanzania kuwapa miradi mikubwa

74191 Wakandaripic

Wed, 4 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya usajili wa Makandarasi (CRB), Consolata Rugimwa ameiomba Serikali ya Tanzania kufanya mchakato wa kubadilisha sheria ili kuwawezesha makandarasi wa ndani kupewa miradi mikubwa inayofanywa na kampuni za nje.

Akizungumza leo Jumatano Septemba 4, 2019 katika mkutano wa mashauriano wa makandarasi, wahandisi na wakadiria majengo jijini Dar es Salaam, Rugimwa amesema, "Serikali ijenge mazingira wezeshi ya kitaalamu ili kushindanisha makandarasi wa nje kwa kushirikisha wataalamu wa ndani.”

"Kwa sasa hakuna sheria. Tunajitahidi kupeleka wataalamu kwenye miradi ya umeme wa mto Rufiji na reli lakini kwa sababu hakuna sheria ni kuomba tu. Hata rates (viwango) vyao ni vidogo.”

Mwenyekiti huyo pia ametaja changamoto ya kukataliwa kwa bima kama dhamana ya mikopo kwenye mabenki, “Tunaomba watumie bima kama dhamana kwa sababu hata afya ya binadamu inatumia bima.”

Awali, mwenyekiti wa Bodi ya wahandisi, Profesa Ninatubu Lema amesema kwa sasa wanajenga jengo refu jijini Dodoma ili kuhamasisha ujenzi wa viwanda.

Rais John Magufuli ndio mgeni rasmi katika mkutano huo uliohudhuriwa na washiriki zaidi ya 4000.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz