Waziri wa Nishati, January Makamba, amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan yuko mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta ya nishati inaimarika kwa lengo la kunufaisha Taifa kiuchumi hasa katika kuvutia wawekezaji.
Makamba amezungumza hayo alipokutana na kuzungumza na mabalozi wa mataifa ya Saudi Arabia, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Algeria nchini Tanzania, kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya Waziri Mkamba imefafanua kuwa mazungumzo hayo yanalenga kuimarisha uhusiano wa kisekta baina ya Tanzania na nchi hizo, ili kuiongezea tija sekta ya nishati kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
Aidha, Mabalozi waliofanya mazungumzo na Makamba ni pamoja na Balozi Abdulaziz, Hamad Alasim (Saudi Arabia), Balozi Hussain Ahmad Al-Homaid (Qatar), Balozi Khalifa, Abdulrahman M.A Almarzooqi (UAE), na Balozi Ahmed Djellal (Algeria)