Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makamba: Hifadhi ya mafuta kimkakati ni usalama wa Taifa

E6bd6295f70c1ba5654cac4c70df3335 January Makamba, Waziri wa Nishati

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Nishati imesema hifadhi ya mafuta ya kimkakati inayotaka kuian-zisha katika mwaka ujao wa fedha wa 2022/2023 ni nyenzo muhimu ya usalama wa Taifa.

Hayo yalibainishwa na Waziri mwenye dhamana, January Makamba wakati akihitimisha hoja yake bungeni Dodoma juzi. Makamba alisema sheria za nchi hii zi-namtaka mtu mwenye ghala la mafuta au kituo cha mafuta awe na ziada ya mafuta ya siku 15 za mbele kwa sababu ya dharura.

Alisema kwenye hiyo kanuni kuna vi-pengele vya kutaka kujikinga na kuwa na hifadhi nchini ikiwa kutatokea dharura.

“Sisi tumeweka siku 15 kwa sababu tu ya uwezo wa hifadhi na uwezo wa mafuta, kuna nchi nyingine zinahifadhi ya siku 90 na nyingine mpaka miezi sita, kwamba ikitokea dharura yoyote, nchi iwe na ma-futa ya kutosha, sisi tumeamua safari hii tufanye mambo yatakayotupeleka zaidi ya siku 15,” alisema.

Alisema hifadhi ya mafuta ya kimkakati siyo lazima iwe eneo maalumu la kuhifadhi mafuta kwenye visima au matangi, bali ni kuifanya Tanzania iwe kituo kikubwa cha biashara ya mafuta ili nchi zote za ukanda huu ziwe zinanunua mafu-ta hapa.

“Hii ndiyo hifadhi ya mafuta ya kimka-kati na sisi tutatumia njia hii ya kuwa na mafuta ya kutosha hapa nchini ili kuibadilisha Tanzania iwe kituo kikubwa cha mafuta katika ukanda huu,” alisema Makamba.

Alisema mtu anaweza kuwa na fedha taslimu, lakini ikitokea dharura hataweza kuyaleta mafuta nchini, hivyo lazima biashara hiyo ifanyike hapa hapa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live