Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makamba: Gesi ya Tanzania tamu

70bd9aa150e88f288570bdf0ee8944e0 : Gesi ya Tanzania tamu

Sun, 12 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia katika mikoa ya Mtwara na Lindi unashindana na miradi mingine mikubwa ya aina hiyo duniani, hivyo wana kazi ya kuweka mazingira mazuri ya kuufanya mradi huo uvutie zaidi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati, Januari Makamba leo Juni 11, 2022 wakati wa utiaji saini makubaliano ya awali ya mkataba wa nchi hodhi (HGA) wa mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia (LNG) ulioshuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dodoma

Amesema upepo wa mafanikio upo pande wa Tanzania kutokana na gesi yake kuwa na kiwango kidogo cha hewa ukaa na salfa ambayo kitaalamu inaitwa ‘gesi tamu’.

“Katika kipindi hiki ambacho dunia inashughulika na tatizo la mabadiliko ya tabianchi, gesi hii ndiyo inayopendwa na kukimbiliwa duniani, hivyo ni turufu kubwa kwa Tanzania kwenye mradi huu.”Amesema Makamba

Pia alitaja sababu nyingine ya upepo wa mafanikio kuwa upande wa Tanzania ni majadiliano ya mabadiliko ya tabianchi duniani ambapo dunia inataka kuondoka katika nishati chafu na kwenda kwenye nishati safi.

Kwa mujibu wa Makamba, gesi asilia ni nishati ya mpito kwa kuwa si safi sana na wala si chafu, hivyo mradi huo umepata turufu nyingine kwa hilo.

“Jingine ni mwenendo wa kijiopolitiki duniani ambapo nchi zinazotumia nishati kwa wingi, sasa hivi zinatafuta vyanzo vipya na vya uhakika vya nishati, na Tanzania imeonekana ni chanzo kipya na cha uhakika cha nishati.” Amesema

Aidha, amesema kijiografia Tanzania itapata mafanikio kutokana na mradi huo kwa kuwa asilimia 70 ya masoko ya gesi yapo katika nchi za Asia ikiwemo China, India, Korea na Japan, hivyo kijiografia ni rahisi kwa Tanzania kuyafikia masoko hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live