Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesimamisha rasmi uchimbaji kokoto katika eneo la machimbo maarufu kwa jina la 'Msingimbio' lililopo Boko mkoani humo
Makalla ametoa maagizo hayo leo Alhamisi Mei 27, 2022 alipofika eneo hilo na kuzungumza na wananchi wanaofanya shughuli zao hapo.
Amesema amefikia hatua hiyo baada ya kufuatilia kwa kina mgogoro huo pamoja na wataalam wa ardhi na kujiridhisha kuwa kampuni ya Alhoom ndio mmiliki halali na ana nyaraka zote.
"Kuanzia sasa nasitisha rasmi shughuli za uchimbaji kokoto eneo hilo kwani baada ya kufuatilia mmebainika nyie ni wavamizi kama wavamizi wengine na mwenye haki hapa ni Alhoom," amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Hata hivyo amewapa ahueni kwa ambao tayari wameshachimba kabeba kokoto zao ndani ya siku saba na baada ya hapo atakayekutwa eneo hilo atakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Pia amesema kutakuwepo na ulinzi wa jeshi la Polisi na kumtaka mwekezaji kama ana walinzi wake naye kuongeza nguvu.
Advertisement "Kuanzia sasa eneo hili litalindwa na polisi na Alhoom kama una walinzi wako Walter hapa waongeze nguvu kwa polisi, maana nimeshatoa maagizo ya kutofanyika shughuli yoyote hapa,” amesema Mkuu huyo.
Ametumia nafasi hiyo kuwaonya watu wanaovamia maeneo ya watu ukaacha tabia hiyo mara moja na kueleza kuwa hilo katika uongozi wake hatalivumilia kwa kuwa kwa ukaacha hivyo tabia hii naweza kuota mizizi na kuwakosesha haki kwenye umiliki halali.
Kwa upande wao wananchi wakinangumza kuhusu hatua hiyo, akiwemo Ester Galaga amesema serikali iwafikirie kwani hawana pa kwenda na hapo ndipo walikuwawa ategemea kupata fedha za kuonyesha maisha yao na familia zao.
"Hii ni nchi yetu, tuende wapi sasa tu apofukuzwa hapa, tuna watoto wanasoma ada tunapatia hapa," amesema.
Eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 70.2 limekuwa na mgogoro kwa takribani miaka 13 jambo lililomfanya mwekezaji huyo kushindwa kujenga kiranda cha saruji.