Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makaa ya mawe yatumike kuzalisha umeme

Makaa Ya Mawe Makaa ya mawe yatumike kuzalisha umeme

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini Antony Mavunde amelitaka Shirika la Madini Tanzania STAMICO kwa kushirikiana na Tanesco kuweka mikakati ya kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe ili kuondoa changamoto ya umeme nchini.

Waziri Mavunde ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika mgodi wa makaa ya mawe Kabulo-Kiwira wilayani Ileje mkoani Songwe akisema rasilimali hiyo itumike kulingana na kasi teknolojia ya dunia inavyokwenda.

Aidha Waziri Mavunde ameainisha kuwa dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuona nchi inajitoshereza kwa nishati ya umeme .

Mgodi wa Kabulo-kiwira una hazina ya makaa ya mawe zaidi ya Tani Milioni 80 .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live