Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaribio SGR Dar- Moro mwezi ujao

Sgr Pic Data Majaribio SGR Dar- Moro mwezi ujao

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema linatarajia mwezi ujao, kuanza majaribio ya kutoa huduma katika Reli ya Kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alisema kazi ya ujenzi wa SGR, awamu ya kwanza kilometa 1,219 kati ya Dar es Salaam na Mwanza na kwamba kipande cha Dar es Salaam – Morogoro kilometa 300 imefikia asilimia 99.77.

Msigwa aliwaeleza waandishi wa habari Dodoma kuwa lipande cha Morogoro – Makutupora kilometa 422 kazi imefikia asilimia 91.79, kipande cha Makutupora – Tabora kilometa 368 kazi imefikia asilimia 3.95 na kipande cha Tabora – Isaka kilometa 165 kazi imeanza.

Alisema kipande cha Isaka – Mwanza kilometa 341 ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 22.71. “Awamu hii ya kwanza pekee inatarajiwa kugharimu Sh trilioni 16. Na kati ya fedha hizo tayari, serikali imeshatoa kuwalipa wakandarasi kiasi cha Sh trilioni 8.143,” alisema.

Alisema awamu ya pili itahusisha kipande cha Tabora – Kigoma, kilometa 506 zinazojumuisha njia kuu za kilometa 411 na mapishano kilometa 95 na kwamba mkataba wa ujenzi umesainiwa na wakandarasi wapo eneo la mradi.

Msigwa alisema kipande cha Uvinza – Msongati – Gitega kilometa 367, mchakato wa ununuzi kwa ajili ya kupata wakandarasi unaendelea na kipande cha Isaka – Rusumo – Kigali, kilometa 365 serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi.

“Huu ni mradi mkubwa ambao sio tu utainufaisha nchi yetu kwa mapato makubwa ya bandari, usafirishaji na ajira bali pia utasaidia kulifungua kibiashara eneo hili la maziwa makuu na hivyo kuboresha maisha ya wananchi,” alisema.

Kuhusu ununuzi wa mabehewa alisema 14 mapya yaliyotengenezwa Korea Kusini yamewasili nchini na yanasubiriwa mabehewa 45.

Alisema vichwa 17 vya treni za umeme na seti za treni aina EMU 10 vinaendelea kutengenezwa Korea Kusini kwa mkataba wa miezi 34 unaogharimu dola za Marekani milioni 295.74 (takribani Sh bilioni 680).

Msigwa lisema pia yameagizwa mabehewa 1,430 ya mizigo kwa mkataba wa unaogharimu dola za Marekani milioni 127.2 (sawa na takribani sh bilioni 292 za Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live