Menu ›
Biashara
Thu, 6 Jul 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo anatarajiwa kuzindua ofisi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) Kanda ya Kusin,i ambayo ipo mkoani Mtwara.
Taarifa ambayo imetolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkoani Mtwara, imesema Majaliwa atawasili mkoani hapa mchana na kuzindua ofisi hizo za TADB zilipo Mjini Mtwara na baadae kuzungumza na wananchi.
Baada ya hapo anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi mkoani Mtwara kwa siku saba kuanzia kesho Julai 7, 2023.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live