Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa ataka ubunifu kuondoa msongamano Tunduma

MALORI 1 780x470 Majaliwa ataka ubunifu kuondoa msongamano Tunduma

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Songwe. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, kubuni mradi wa maegesho ya malori ili kupunguza msongamano uliopo katika Mji wa Tunduma.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Novemba 24, 2023 aliposimama kuwasalimia wananchi wa Jimbo la Vwawa ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake Mkoa wa Songwe katika Wilaya ya Ileje na Mbozi .

Amesema umefika wakati wataalamu watumie uwezo wao wote kufanya Mji wa Vwawa kuwa pumulio la msongamano uliopo Tunduma hivi sasa.

“Nimewaagiza wataalamu kutafuta eneo ambalo wanaweza kujenga maegesho ili madereva wa malori waweze kupumzika wakati wanasubiri kuvuka mpaka wa Tunduma sambamba ujenzi wa nyumba za kutosha za kulala wageni zitakazo chochea mapato ya Serikali.

Awali, Mbunge wa Vwawa (CCM), Japhet Hasunga, ameomba kujengwa stendi kubwa ya kisasa, soko la mazao la kimataifa ili wakulima waweze kulitumia kuuza mazao yao kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi badala ya kuwaacha waende hadi mashambani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live