Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa aituliza Kariakoo biashara kurejea!

Majaliwa: Tekelezeni Miradi Kwa Fedha Za Ndani Majaliwa aituliza Kariakoo biashara kurejea!

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mkutano na, Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo ambao mapema leo waligoma kufungua maduka yao na kushinikiza kutaka kukutana na Rais, Samia Suluhu Hassan kwa madai ya kulipishwa kodi kubwa na Mamlaka ya Mapato nchi (TRA).

Akizungumza katika Soko la Kariakoo, leo Mei 15, 2023 Waziri Majaliwa amewaomba wafanyabiashara hao kufungua maduka hayo ili waendelee na biashara zao kwa sababu kariakoo ni soko la kimataifa hivyo nchi isije kupoteza wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kwa kuona Tanzania ni sumbufu.

“Naomba niwahisi mkubali ombi la Serikali, fungueni maduka, mrudi mfungue maduka wataje wapo, nina sababu mbili, ya kwanza Soko hili ni la kimataifa tusipoteze wafanyabiashara kutoka nje kwa kuona Tanzania ni sumbufu, mbili tunajua kero hizi zinafanywa na watu wetu tuliowapa dhamana tuachieni tukiwabaini tutawashughulikia,” amesema Waziri Majaliwa.

Hata hivyo Mwenyeketi wa wafanya biashara hao ameitikia wito kwa naiaba ya wenzanke wote hivyo biashara katika soko hilo la kimataifa zitarejea upya huku wakisubiri mwarobaini wa changamoto zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live