Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa: Wakulima wafugaji waeleweshwe ilipo mitaji

FEDHA WEB Majaliwa: Wakulima wafugaji waeleweshwe ilipo mitaji

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo iweke katika lugha rahisi andiko juu ya upatikanaji wa mitaji na pembejeo kwa wakulima na wafugaji.

“Niendelee kuzitaka Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ziandae utaratibu wa kuziweka kwenye mifumo rahisi na kuzifikisha kwa wakulima na wavuvi maelezo juu ya upatikanaji wa mitaji, kupata pembejeo kwa urahisi na kuifikia teknolojia mpya.”

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Agosti 3, 2023) baada ya kukagua mabanda ya Maonesho ya Nane Nane Kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.

Akizungumza na wadau na washiriki wa maonesho hayo, Waziri Mkuu amesema akiwa ziarani Urusi, wiki iliyopita alikutana na mwekezaji wa mbolea ambaye anataka kuja kuwekeza nchini. “Bado mahitaji ya mbolea ni makubwa, bado tuna mahitaji ya masoko na teknolojia kwa wavuvi na wakulima. Elimu iendelee kusambazwa juu ya upatikanaji wa mbolea,” amesisitiza.

Akielezea kuhusu maonesho hayo, Waziri Mkuu amesema maonesho ya mwaka huu ni mazuri zaidi ya mwaka jana kwani ameona kuna teknolojia nyingi mpya ambazo zimebuniwa na vijana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live