Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa: Wajasiriamali wasibanwe

Majaliwa Amuagiza RC, RPC Wamkamate Mzazi Anayedaiwa Kumlawiti Mwanaye.jpeg Majaliwa: Wajasiriamali wasibanwe

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza viongozi wa Mkoa wa Simiyu wasiwabane wajasiriamali, wawaelimishe na kuwapa miongozo ili wajiendeleze kiuchumi.

Majaliwa alitoa agizo hilo jana asubuhi wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Mji wa Bariadi katika eneo la stendi ya zamani akiwa njiani kwenda Maswa.

Alitoa kauli hiyo akilenga biashara ya usafirishaji wa abiria kwa kutumia magari madogo aina ya probox ambayo yalikuwa yamezuiliwa na uongozi wa mkoa huo.

“Viongozi nimewaomba msiwabane vijana wajasiriamali, msiwazuie kujiendeleza kiuchumi, cha msingi wapeni miongozo, wapeni elimu. Na vijana ni lazima mzigatie usalama wa gari na abiria na kufuata sheria zilizowekwa,” alisema Majaliwa na kuongeza:

“Mkuu wa Mkoa, ofisi yako ilisitisha matumizi ya magari haya maarufu kwa jina la mchomoko na sasa tumefungua milango. Mheshimiwa Rais wetu, Samia Suluhu Hassan alikwishaelekeza kuwa hawa wajasiamali wadogo wawezeshwe.” Pia ameagiza stendi kuu ya mabasi katika mji wa Bariadi mkoani humo ianze kutumika kwa mabasi makubwa na madogo ili kuondoa usumbufu kwa abiria.

“Mkuu wa Mkoa wekeni utaratibu utakaofaa ili mabasi yaanzie pale na kuishia pale lakini haimaanishi kuwa muwapitilize abiria wanaoshukia au kupandia njlani,” alisema Majaliwa.

Aliongeza: “Jana nilitembelea pale stendi kuu na kuona fedha za Serikali zinapotea bure. Kuna vibanda 148 vya wajasiriamali lakini hawafanyi kazi kwa sababu hakuna abiria wanaoingia na kutoka.

“Kuna vijanawa bajaj na bodaboda wamejipanga vizuri lakini hawana kazi kwa sababu hakunamabasi”. Amesema serikali ilitoa Sh bilioni saba zitumike kuupanga Mji wa Bariadi na pia ikaanzisha mfumo wa anuani za makazi ili uwepo urahisi wa kufikika. Majaliwa amesema kuwepomalori katika eneo hilo kutafungua ajira kwa vijana mafundi wa magari, mafundi umeme,wauza vipuri na mafundi gereji.

“Wote waende kule na Halmashauri waboreshe lile eneo kwa kuweka huduma zote za msingi,” amesema.

Majaliwa ameagiza madereva wa magari hayo wafanye usajili katika Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na kwa maofisa biashara na wazingatie sheria zza usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kupakia abiria sawa na uwezo wa chombo hicho.

“Jeshi la Polisi nendeni mkatoe elimu ili watu wafanye biashara kwa kufuata sheria. “Tukiacha mambo yaende holela, tutajikuta tunatengeneza utamaduni ambao utawakwaza ninyi na wao pia watakwazika,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live