Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa: Uwekezaji ATCL uchochee ukuaji uchumi

ATCL ATCL CARGO TATU.jpeg Majaliwa: Uwekezaji ATCL uchochee ukuaji uchumi

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Uchukuzi kuisimamia ipasavyo Kampuni ya Ndege Tanzania ,(ATCL) ili kuhakikisha uwekezaji mkubwa uliofanywa ndani ya kampuni hiyo unaleta matokeo chanya na kuwa kichocheo cha ukuaji wa sekta nyingine mtambuka na uchumi kwa ujumla.

Amesema kuwa ongezeko la ndege na huduma za usafiri linasaidia kuongeza fursa za biashara kati ya Tanzania na mataifa mengine, kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni na kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania.

Waziri Mkuu amesema hayo mkoani Dar es Salaam leo Machi 26, 2024 wakati wa mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 737-9 Max kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Amesema ili kuendelea kukuza sekta ya anga nchini, Wizara ya Uchukuzi iandae mpango wa kuongeza wataalamu wazalendo katika fani zinazohusu masuala ya ndege hususani kwenye eneo la matengenezo na urubani.

Waziri Mkuu pia amewaagiza watumishi wa ATCL kuongeza uzalendo na kuwafichua watu wote wenye nia ya kuihujumu kampuni hiyo pamoja na kudhibiti upotevu wa mapato kupitia tiketi na mizigo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live