Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa: Mvua nyingi chanzo upungufu wa sukari nchini

Sukarii Sukari Leseni Majaliwa: Mvua nyingi chanzo upungufu wa sukari nchini

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema changamoto ya uhaba wa sukari nchini imetokana na athari za mvua nyingi zilizopelekea maeneo ya mashamba ya miwa kufurikwa maji kiasi kwamba wamiliki wa mashamba ya miwa wameshindwa kuvuna miwa kupeleka kiwandani.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya katika kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu.

Ameongeza kuwa wizara ta Kilimo imetoa vibali kwa Wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wazalishaji wa sukari kuingiza sukari nchini zaidi ya tani laki moja.

Waziri Mkuu amesema taarifa zilizopo hadi sasa ni kwamba sukari imekwishaingia na Watanzania wataweza kuitumia bidhaa hiyo.

Katika swali lake kwa Waziri Mkuu Mhandisi Manyanya aliuliza kuwa pamoja na jitihada za Serikali kuhakikisha nchi inakuwa na sukari muda wote, katika siku za karibuni kumekuwa na taharuki ya upungufu wa sukari na ikizingatiwa kipindi cha karibuni kutakuwa na mfungo wa Kwaresma na Ramadhani, na kutaka kujua kauli ya Serikali kuwatoa Wananchi hofu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live