Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa: Msamaha wa ruzuku hutolewa kwa umuhimu

89586592 908x640 Msamaha wa ruzuku hutolewa kwa umuh

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imekuwa ikitoa misamaha au ruzuku pale inapojiridhisha kuwa panahitajika kufanya hivyo, akitolea mfano wa hivi karibuni baada ya mbolea kupanda bei ilitoa ruzuku ya shilingi bilioni 150 kwenye mbolea ili kuhakikisha bidhaa hiyo inapatikana kwa wakulima kwa gharama nafuu.

Majaliwa ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Zaituni Swai aliyetaka kujua mikakati ya Serikali katika udhibiti wa bei ya soko pale misamaha inapotolewa.

Amesema, Serikali itahakikisha maeneo yote yanayopata misamaha au ruzuku yanasimamiwa kwa ukaribu, ili kudhibiti mfumuko wa bei na kwamba suala la ucheleweshwaji wa fidia kwa wananchi ambao maeneo yao yamechukuliwa kwa ajili ya kupisha miradi mbalimbali ya maendeleo linatokana na taratibu zinazotakiwa kufuatwa kabla ya ulipaji wa fidia ikiwemo kujiridhisha ni nani mmiliki sahihi wa eneo husika.

Waziri Mkuu amesema, wananchi wote waliochukuliwa maeneo yao kupisha ujenzi wa miradi ya maeneleo watalipwa stahiki zao ikiwa ni jibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini, Kirumbe Ng’enda aliyetaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu ucheleweshaji wa ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaochukuliwa maendeo yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live