Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majadiliano COP28 kuziwezesha jamii za wafugaji

Jamii Wafugaji Majadiliano COP28 kuziwezesha jamii za wafugaji

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika harakati za kuleta mabadiliko chanya na uwezeshaji wa kifedha kwa wananchi wake, Serikali ya Tanzania imetengeneza ushirikiano wa kimkakati na taasisi za ndani na za kimataifa.

Ushirikiano huu unalenga kutengeneza uwezo wa kuingiza mapato kutokana na shughuli mbalimbali huku Carbon Tanzania ikionekana kuwa tumaini la mabadiliko chanya haswa kwa jamii za asili.

Katika ushirikiano huu, mkutano wa COP28 unaoendelea Dubai umewakutanisha viongozi wa dunia kujadili mikakati muhimu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Majadiliano ya COP28 yanasisitiza uharaka wa kupata suluhisho za kibunifu, hasa zile zinazohusisha na kunufaisha jamii za asili kama ulinzi wa mazingira.

Isack Bryson, Meneja wa Mradi wa Bonde la Yaeda-Eyasi, anaeleza alichokishuhudia katika mkutano wa COP28: “COP28 inaongelewa sana kila mahali na imeleta matumaini makubwa kwangu na jamii yangu hata kabla sijaja leo. Tunatumai kwamba kupitia kushirikishana kuhusu athari za mabadiliko ya tabinchi, njia za kukabiliana na changamoto hiyo zitatolewa hivi karibuni ulimwenguni kote kwa maisha bora na hali ya hewa inayofaa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live