Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maharage ya Jesca yaongezewa thamani, kutengenezea keki, biskuti!

WhatsApp Image 2022 08 07 At 7.jpeg Maharage ya Jesca yaongezewa thamani, kutengenezea keki, biskuti!

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watafiti kutoka Kituo cha utafiti cha Tari Seliani wameanza kuyaongezea thamani maharage ya Jesca kutokana na madini chuma na Zinki yaliyopo kwenye maharage hayo kwa kutengeneza aina mbalimbali za vyakula vinavyotokana na maharage hayo.

Hayo yamebainika wakati wa maonyesho ya wakulima na mifugo nanenane yanayofanyika kwa kanda ya kaskazini ikijumuisha mikoa ya Kilimanjaro,Tanga,Manyara na Arusha ambao ndiyo wenyeji wa maonyesho hayo.

Aidha watafiti hao wanasema katika kuongezea thamani maharage hayo ya Jesca kwa sasa wameweza kutengeneza Biskuti,Keki na Mikate inayotokana na maharage hayo ili kuendelea kuupa thamani unga huo.

Salome Munis ni mtafiti muandamizi kutoka Tari Seliani ambapo anasema maharage hayo yanaweza kubadilisha maisha ya watanzania kuweza kuacha kutumia vyakula vyenye wanga na badala yake kutumia vyakula vyenye protini zaidi ikiwemo maharage hayo.

Akiainisha baadhi ya aina ya mazao waliotafiti amesema Kwa sasa mbali na maharage ya Jesca pia wametafiti mazao ya ngano, shayiri ambayo yameweza kupokelewa vizuri na jamii.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Tari Felista Madon wamepongeza hatua hiyo kwa kuwa hawatakuwa na changamoto ya utumiaji vyakula vya wanga.

Wakazi wa Kanda ya kaskazini wameendelea kutembelea maonyesho ya kilimo na mifugo kujionea bidhaa mbalimbali kwenye maonyesho hayo yenye kauli mbiu kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,mifugo na uvuvi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live