Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Kuu yasimamisha tozo za miamala ya simu, benki

Miamala Benkii Mahakama Kuu yasimamisha tozo za miamala ya simu, benki

Sat, 14 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu nchini Kenya imesimamisha ada ya kutuma pesa kutoka kwa akaunti yako ya benki hadi kwa simu - ada iliyorejeshwa majuzi baada ya takriban miaka mitatu.

Katika uamuzi wake mnamo Alhamisi - Januari 12 - Jaji Mugure Thande aliagiza kampuni za mawasiliano na Benki Kuu ya Kenya kusimamisha tozo hizo zilizorejea tangu Januari 1, 2023.

Jaji Thande alitoa agizo hilo kesi iliyowasilishwa na mwanaharakati Moses Wafula ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa. Wafula anahoji kuwa serikali ya Rais William Ruto ilikosea kurejesha ada hiyo.

"Mlalamishi anahoji kuwa haki zake na haki za raia wengine zimehujumiwa na zinaendelea kutishiwa na mtuhumiwa wa kwanza na serikali ya Kenya," sehemu ya stakabadhi za mahakama inasema.

Katika rufaa yake, Wafula anahoji kuwa kampuni za mawasiliano zitawalemaza Wakenya ambao tayari wanakandamizwa na gharama ya juu ya maisha.

Kesi hiyo itatajwa Januari 23 huku Jaji Thande akiwataka watuhumiwa wote kujibu tuhuma zao kwa hati ya kiapo ifikapo Januari 20 ili kuwapa walalamishi muda tosha wa kupitia stakabadhi hizo.

Kwa mujibu wa Wafula, Mahakamu Kuu ina nafasi bora zaidi kuwaokoa Wakenya kutoka kwa ada zinazowatesa wakati mustakabali wa uchumi wa taifa unazidi kuyumba.

Ada hizo zilitolewa mwaka 2020 na aliyekuwa rais kwa wakati huo Uhuru Kenyatta ili kuwakinga Wakenya kutokana na athari za janga la Korona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live