Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Kuu kutoa uamuzi kesi ya ving’amuzi Iringa leo

15443 Kingamuzi+pic TanzaniaWeb

Tue, 4 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imeahirisha kupokea maombi ya kesi ya kupinga kuondolewa kwa chaneli za ndani kwenye ving’amuzi vya Azam, Dstv, Zuku na Star times iliyofunguliwa na watu watano, badala yake itatoa uamuzi leo.

Jaji Penterine Kente anayesikiliza kesi hiyo jana alilazimika kuahirisha shauri hilo kwa dakika 20.

Uamuzi huo aliufanya baada ya kutokea ubishani wa kisheria baina ya mawakili wa upande wa waleta maombi na wakili wa Serikali aliyetaka mahakama itoe muda mpaka walalamikiwa wengine watakapokuwepo mahakamani, jambo lililopingwa na mawakili wa upande wa waleta maombi.

Baada ya mabishano hayo, Jaji Kente aliamua kutoa muda wa dakika 20 ili kila upande ukaweke vizuri hoja zao na waliporejea baada ya muda huo, aliamua kuahirisha kesi hiyo hadi leo.

Katika kesi hiyo, waleta maombi Silvanus Kigomba, Jesca Msambatavangu, Oliver Motto, Sebastian Emmanuel Atilio na Hamdun Abdallah wanaiomba mahakama kubatilisha amri ya kuondolewa chaneli za ndani kwenye ving’amuzi vya kampuni hizo.

Wanadai tayari ving’amuzi hivyo vimeshatumiwa muda mrefu na wananchi ambao walivinunua baada ya kuamini kuwa watapata huduma ya kutazama maudhui yanayorushwa na chaneli za ndani.

Katika kesi hiyo namba moja ya mwaka 2018, waleta maombi wanawakilishwa na mawakili Chance Luwoga na Edmund Mkwata.

Chanzo: mwananchi.co.tz