Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magunia milioni mbili yatengwa kufungashia korosho ghafi

Hji Magunia milioni mbili yatengwa kufungashia korosho ghafi

Thu, 20 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Idadi hiyo ya magunia ya kufungia korosho ni mbali na magunia laki saba yaliyobaki katika msimu wa 2021,ambayo itafanya jumla ya magunia yote kwa msimu wa 2021/2022 kuwa milioni 3.5.

 Kauli hiyo imetolewa leo wilayani Tandahimba mkoani Mtwara na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, Francis Alfred, wakati wa uzinduzi wa mpango rasmi wa usambazaji wa pembejeo na matumizi sahihi ya viuatilifu kwa mazao ya korosho kwenye mkoa huo.

Mbali na magunia ya kufungashia korosho, Alfred amesema wanatarajia kusambaza tani 21,000 ya Salfa ya Unga,Viuatilifu vya ugonjwa wa ubwiri unga lita 528,000,Viuatilifu vya ugonjwa wa blati lita 578,000, huku usambazaji wa viuatilifu vya wadudu waharibifu ikiwa ni lita 300,000.

 Asema usambazaji wa pembejeo na magunia utafanywa na makampuni wazabuni, waliofunga mikataba na Chama Kikuu cha Ushirika kutoka Wilaya za Mtwara, Nanyumbu,Masasi na Newala (MAMCU), kwa niaba ya vyama vingine vya ushirika. Na kwamba usambazaji huo wa pembejeo ulianza Mei 15 mwaka huu, huku ule wa magunia ukitarajiwa kuanza agosti thelathini mwaka huu.

 Amesema ununuzi wa pembejeo na magunia umezingatia makadirio ya uzalishaji korosho ghafi tani 230,000  katika msimu wa 2021/2022.

 “Kwa utaratibu huu wa mjengeko wa bei, mkulima atakayepatiwa viuatilifu atachangia  kiasi cha shilingi 110.54 kwa kila kilo atakayouza huku mnunuzi akichangia gharama ya pembejeo na magunia jumla kwa shilingi 165.11 kwa kila kilo”amesema Alfred.

Chanzo: ippmedia.com