Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli ataja kiini cha mapato hafifu

Wed, 10 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema mfumo wa ukusanyaji kodi nchini ni sehemu ya  sababu za ukusanyaji wa mapato kidogo kutoka kwa Watanzania na kueleza atakabiliana na dosari hizo ili kupanua wigo na idadi ya walipa kodi nchini.

Amesema nchi zilizoendelea duniani zimekuwa zikitoa adhabu kali kwa wanaokwepa kulipa kodi kwa lengo la kukatisha tamaa wanaojihusisha na vitendo hivyo. 

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha majani ya chai katika kijiji cha mkoani Njombe, ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mikoa mbalimbali nchini.

“Kwa hapa nchini ukusanyaji wa kodi uko chini mno, ni watu milioni 2.7 kati ya watu milioni 55 ndiyo wanalipa kodi, kwa hiyo tuna matatizo katika mfumo wetu wa kukusanya kodi, kuna matatizo kwa watendaji wetu wakiwamo TRA, tuna matatizo kwa baadhi ya wawekezaji wanaotaka kupata super profit( faida kubwa).”

“Kwa hiyo ni mchanganyiko wa mambo mengi, sisi kama taifa lazima tuyafanyie kazi. Mimi pamoja na mawaziri wa viwanda, kilimo pamoja na wabunge tuangalie mikakati iliyo bora zaidi, watu wasitozwe kodi za kuonea. Ukifanya hivyo unam-discourage( katisha tamaa) yule aliyekuja kuwekeza,” amsema Rais Magufuli.



Chanzo: mwananchi.co.tz