Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli ashangazwa TTCL kukodi minara kwa Sh700milioni kila mwezi

58836 Pic+magufuli

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ameshangazwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kutokuwa na minara yake na hivyo kutumia minara ya mashirika mengine kwa kulipia kati ya Sh700milioni hadi Sh800milioni kila mwezi.

Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 21, 2019 katika hafla ya shirika hilo kutoa gawio kwa Serikali iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa awamu ya pili ya huduma ya video conference.

Amesema walipokutana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alimuuliza mfuko wa mawasiliano kwa wote ni wa nani na kujibiwa uko chini ya wizara yake ikiwa na maana kuwa ni fedha za wananchi huku pia TTCL ni shirika la wananchi.

“Wakati una mfuko wa mawasiliano unaojenga minara kila sehemu kwa nini usijenge minara ukawapa TTCL, kwa sababu ni kweli kuwa mashirika mengine yanachangia kwa kulipa kodi lakini hawa wanalipa kodi na kutoa gawio na faida inayopatikana ni ya nchi hii.”

“Ninajua wajumbe wa kamati ya miundombinu na uwekezaji mko hapa, waziri upo na katibu mkuu, hakuna sababu ya kuiumiza TTCL kuhangaika kukodi minara kwa watu wengine. Unamuacha mtoto wako ahangaike kutafuta chakula wakati unacho na unakigawa kwa haohao,” amesema Magufuli.

Ameongeza, “Ni matumaini yangu wizara inayohusika sasa hili mliangalie kuwa TTCL ni lazima tuwape mtaji na wa kuwapa ni sisi tusidanganyike hawatakuja watu wa kutusaidia. Hawatatokea na hawajawahi kutokea duniani, ni lazima mashirika kama haya ambayo ni mali za Watanzania zipewe kipaumbele.”

Habari zinazohusiana na hii

Chanzo: mwananchi.co.tz