Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli : Maduka ya kubadilishia fedha yalikuwa uchochoro wa kusafirisha fedha chafu

49209 Raispic

Thu, 28 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema maduka ya kubadilishia fedha nchini yaliyokuwa yakifunguliwa kama uyoga yalikuwa uchochoro wa kusafirisha fedha chafu nje ya nchi.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akimuapisha Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Valentino Mloweza na kupokea taarifa ya kazi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Amesema watu walikuwa wakiiba fedha Benki Kuu (BOT) na kwenda kuuza kwenye maduka ya kubadilishia fedha, lakini wakiulizwa hawakuwa wanasema wameuza kiasi gani.

Amesema hakukuwa na ripoti yoyote inayoonyesha wameuza kiasi gani cha fedha na kwamba suala hilo ilikuwa utapeli na kutikisa uchumi wa nchi.

“Na wakishatoka kule wanatumia ‘exchange bureau moja (duka moja la kubadilishia fedha) wanamuuzia mtu wao kwa bei ya Sh1,400.”

“Na wanachukua hiyo ‘cotation’ kwamba ‘exchange ya TSh (fedha ya Tanzania) imepanda juu na ile ni kudistable (athiri) uchumi wa nchi, nikamwambia gavana hebu kafanye kazi moja huko,” amesema.

Related Content

Amesema  japo walifika Sh2400 baada ya maagizo yake  lakini haijatokea tena suala hilo.

“Ulikuwa utapeli tu kutikisa uchumi wetu, nikimuuliza wewe kweli huna dola huku mzee, anasema ninazo nyingi mno. Fedha zipo hata za reserve (akiba) zipo, nchi inaweza kuishi zaidi ya miezi mitano bila kukusanya fedha yoyote.”

“Wizi wa ajabu umekuwa ukifanywa na zile ‘transactions’ (miamala) za ajabu bila utaratibu, hakuna nchi nenda hata zilizoendelea, mimi nilienda Ujerumani mpaka nilitoa passport (hati ya kusafiria) kubadilisha fedha mpaka askari anaangalia natembeaje na dola 2,000,” amesema.

Rais Magufuli amesema fedha za dawa za kulevya pia zimekuwa zikipita huko (maduka ya kubadilishia fedha).

 



Chanzo: mwananchi.co.tz